Rais wa Marekani, Donald Trump amesema Serikali za majimbo nchini humo zinapaswa kufikiria kufungua shule za umma ili wanafunzi waendelee na masomo.
Ametoa kauli hiyo katika mkutano kwa njia ya simu na Magavana walipokuwa wakijadili jinsi ya kuruhusu tena shughuli za kiuchumi kuendelea.
Hata hivyo, kwa mujibu wa Shirika la Associated Press, hakuna Gavana yeyote aliyeridhia pendekezo hilo la kufungua shule. Maafisa wengi wa elimu wana wasiwasi kuwa huenda kukawa na hasara kubwa hata kuliko faida.
Shule zote nchini humo zilifungwa kutokana na tishio la #COVID19 ambapo hadi sasa, Marekani ina jumla ya visa 1,035,765 na vifo 59266 vilivyotokana na #CoronaVirus.