RC Makonda: Hali ya Maambukizi ya Virusi vya Corona Ndani ya Dar Siyo Nzuri Msiwaruhusu Ndugu zenu Kutoka Mkoani Kuja Huku



Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewaombea radhi wakazi wa Jiji hilo kwa ndugu zao walioko mikoani, ambao wanatamani kuja jijini humo, kwamba wasiwaruhusu kutoka huko waliko kwa kuwa hali ya maambukizi ya Virusi vya Corona ndani ya Dar es Salaam siyo nzuri.

Makonda ameyabainisha hayo leo wakati akipokea msaada wa vifaa vyenye thamani ya Shilingi Bilioni 1 vilivyotolewa na mfanyabiashara Rostam Azizi.

"Niwaombee radhi wananchi wa Dar es Salaam, ukiona ndugu yako anakupigia simu anataka kuja huku mwambie uliona tangazo la RC siku hizi wanapita nyumba kwa nyumba kukagua wageni muache anilaumu ili wote muwe salama maambukizi ya mkoa wetu hayafurahishi sana" amesema Makonda.

Aidha Makonda amewashangaa wale watu wanaodhani kuwa maambukizi ya Virusi vya Corona ni kwa ajili ya Serikali pekee.
"Wako watu wanafikiri Corona ni kwa ajili ya Serikali, kuna wakati najiuliza hivi watu mpaka augue mtu nyumbani kwake ndiyo ajue huu ugonjwa ni hatari? ukiona Rostam anatoa zaidi ya Bil.1 sio kama ana hela nyingi sema hataki kuona watu wakifa".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad