MwanaHipHop Roma Mkatoliki ameeleza kuwa siku ya Aprili 5,2017, hataweza kuisahau kwenye maisha yake kwani lilitokea tukio la kutekwa na watu wasiojulikana akiwa na msanii Moni Centrozone, producer Bin Laden na Emma.
Roma amesema imepita miaka mitatu sasa, tangu kutokea kwa tukio hilo ila anamshukuru Mungu kwa kumpa nafasi nyingine ya kuishi.
Akikumbuka tukio hilo la kutekwa kwake msanii huyo, ametumia mtandao wa Twitter kwa kuandika "Tarehe kama ya leo Aprili 5, ni miaka mitatu sasa imepita, nakumbuka ilikuwa Jumatano saa 11 Jioni, nikiwa studio Tongwe Records Masaki , na wadogo zangu Moni, BinLaden na Emma sitasahau, Mungu ana kila sababu ya kutupa nafasi nyingine ya kuishi"
Baada ya kutekwa na watu wasiojulikana siku hiyo ya Aprili 5, 2017 alipatikana siku ya Aprili 9 ambapo alikutwa na ana alama za makovu katika mwili wake, hali iliyoashiria mahali alipokuwepo hapakuwa salama kwake