Meneja wa Diamond Platnumz Ashangazwa na Watu Wanaomkashifu Baada ya Kupungua Uzito Kutoka na Ugonjwa wa Corona


Sallam Mendez ni meneja wa msanii wa bongo Diamond. Sallam alikuwa na virusi vya corona na kisha kupona wiki kadhaa zilizopita.

Baada ya kutibiwa, alirudi kupimwa kwa mara mbili na kupatikana hana virusi hivyo.


Mashabiki wake hawakumzoea Sallam kama vile alivyokuwa kwa kupunguza kilo na kukonda kwake.

Kupitia mtandao wake wa kijamii alikuwa na haya ya kusema,

“SASA NILIPOKUWA MNENE OOOH BONGE… CORONA IMENIKONDESHA OOOH MWILI WOTE KWISHA.” Aliandika Sallam.

Diamond hakukimya bali alikuwa na maoni na kumwambia kuwa amebakisha ndevu pekee

“UMEBAKI NDEVU.”Diamond Alisema.

Awali, kuna uvumi ulioendelea kuwa Sallam ameondoka katika lebo ya WCB huku akikana madai haya kupitia mtandao wa kijamii wa instagram

“I DON’T HAVE ANY PROBLEM WITH WCB, WHETHER ITS DIAMOND, RAYVANNY OR ANYONE.
WE WILL CONTINUE TO BE ONE FAMILY. WATCH OUT FOR MORE PROJECTS.”Alisema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad