MTENDAJI Mkuu wa Chama cha Makocha wa Ligi England, Richard Bevan, amesema msimu wa soka nchini humo hautaendelea kama wachezaji wote hawatapimwa corona.
Kauli hiyo inawagusa wachezaji wote kuanzia ligi kuu maarufu Premier ambapo Mtanzania, Mbwana Samatta anaichezea Aston Villa, hadi ligi za chini.Bevan ameiambia BBC Sport kuwa: “Suala la kufanyiwa vipimo ni muhimu kwanza kabla ya mambo mengine kuendelea.”
Hivi sasa ligi mbali mbali duniani zime simama kutokana na janga la Corona.Bosi huyo wa makocha amesema anachoangalia kwa sasa ni kuzungumza na viongozi wa soka nchini humo kuona namna gani msimu unaendelea.“Jambo zuri ni kuona kila mmoja wetu akiwa na afya njema.
“Bado hatujajua ni lini hasa ligi zetu zitarudi tena, pengine tusubiri hadi mwisho wa Aprili hali itakuwaje.“Makocha wetu hawataki kurudi uwanjani hadi wachezaji wafanyiwe vipimo kwanza. Lakini pia tutasububiri kauli ya serikali juu ya kinachoendelea”.