Serikali Dar Yazifunga Baa Kiaina Sababu ya Corona, Marufuku Kunywea Baa



Mkuu wa Wilaya ya Ilala Sophia Mjema amewatangazia wamiliki wa Baa kuwa kuanzia Aprili 17, 2020 hairuhusiwi watu kukusanyika Baa ikiwa ni hatua ya kukubili kuenenea kwa virusi vya Corona.

Katika tangazo lake kwa wananchi wa wilaya hiyo Mjema amesema pombe zitaruhusiwa kuuzwa lakini mununzi ataenda kunywea nyumbani kwake sio kunywea baa.

Clouds Media on Twitter:
"Mkuu wa wilaya ya Ilala Mh. Sophia mjema ...Mjema amesema ni wajibu wa kila mmoja kuzingatia maelekezo hayo kwani hatua za kisheria zitachukuliwa kwa mmliki, mwendeshaji na mtu atakayeonekeana eneo la baa akiendelea kunywa.

Mpaka sasa nchini Tanzania idadi ya visa vya Corona ni 147, waliofariki ni 5 na waliopona ni 11.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad