Serikali Kuajiri Watumishi Wapya Zaidi ya 44,000


Serikali  inatarajia kuajiri watumishi wapya 44,811 katika mwaka wa fedha 2020/2021.

Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Mkuchika ameyasema hayo jana  Jumatano Aprili 15, 2020 wakati akiwasilisha bajeti yake kwa mwaka huo wa fedha.

Ametaja ajira hizo mpya kuwa ni kada ya elimu (13,529), afya (10,467), kilimo, mifugo na uvuvi (2,145) Jeshi la Polisi (2,725), magereza (685), Jeshi la zimamoto (501), uhamiaji (495) na hospitali za mashirika ya kidini na hiyari (1,262).

Aidha, amesema Serikali inatarajia kuajiri watumishi 13,002 wa kada nyingine zikiwamo za wahadhiri wa vyuo vikuu vya umma nchini.

Mkuchika amesema pia Serikali itawapandisha vyeo watumishi 222,290 wa kada mbalimbali kulingana na maelekezo yatakayotolewa.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad