Serikali yakemea Trafiki Kujificha Vichakani na Kupiga Picha za Magari kwa Simu




Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, George Simbachawene amelitaka jeshi la polisi nchini kutumia mbinu za kistaarabu kusimamia sheria za usalama barabarani na kuacha tabia ya kujificha na kuwashtukiza madereva wanaoendesha magari kwa mwendokasi.

Pia ameongeza kuwa utaratibu wa polisi kutumia simu kupiga picha magari yanayokwenda kasi haukubaliki kwa sababu kuna kifaa maalum cha kufanya kazi hiyo.

“Huyu ana Nokia, huyu ana iPhone, huyu ana Samsung, tunaaminianaje, kwamba ni kitendea kazi ambacho tumekipitisha kisheria. Hii haikubali,” amesema.

Simbachawene ameyasema hayo bungeni Dodoma wakati akiwasilisha makadirio ya matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2020/2021, ambapo amesema vitendo vya polisi kujificha na kuvizia magari, vinaweza kupelekea wao wenyewe kugongwa.

“Kwanini tujifiche? Maana barabarani tupo kila siku, na sisi ndio madereva, sioni sababu ya kujificha. Spidi ziko barabarani mule, tuendelee kuongeza elimu zaidi kwa madereva wetu wapate uelewa na kufuata alama za barabarani,” amesisitiza Simbachawene.

Aidha, amemugiza IGP Simon Sirro kutoa maelekezo maalum juu ya udhibiti wa mwendo wa barabarani kwa sababu kinachofanyika sasa kinaleta fujo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad