Shame on you....Mutua Awakashifu Wanasayansi wa KENYA "Nini Mnasubiri Kupata Dawa ya Corona"


Ni nini  ambacho wanasayansi na maprofesa wa humu nchini wanafanya kuhusiana na homa ya Corona? Wanasubiri wengine wafanye utafiti wa kupata dawa ya kutibu Corona?

Hayo ni maneno ya gavana wa Machakos Alfred Mutua ambaye amewakashifu wanasayansi na maprofesa wa humu nchini kwa kile amesema ni kulaza damu wakati wanasayansi kutoka mataifa mengine wanaendelea kufanya utafiti wa kupata tiba ya kutibu ugonjwa COVID 19.

Kufikia sasa, taifa la Kenya limesajili visa 59 vya watu ambao wameathirika na virusi hivyo baada ya kutangazwa kwa mara ya kwanza nchini mnamo Machi 13.

Kufikia sasa, watu zaidi ya alfu 40,000 kote ulimwenguni wameripotiwa kupoteza maisha yao na wengine 800,000 wakiwa wameambukizwa.


Katika video iliyozagaa kwenye mitandao yake ya kijamii Gavana huyo aliwataka wanasayansi na wahadhiri wakuu [professors] kuzinduka kutoka kwenye usingizi na kutafuta mbinu ya kupata kinga dhidi ya virusi vya Corona.

Mutua amekashifu hatua ya taifa hili kuendelea kuagiza dawa kutoka mataifa ya kigeni ilhali kuna uwezo wa Kenya kuanzisha vituo vya kutengeneza dawa humu nchini.

Usemi wake unajiri saa chache tu baada ya mhudumu wa afya kupatikana na virusi vya Corona kaunti ya Nairobi na kulazwa katika kituo kikuu cha kitaifa cha Mbagathi akiwa na mumewe .

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad