MSANII wa filamu Bongo, Shamsa Ford amesema kuwa anaijua thamani yake kama mwanamke, hivyo hawezi kuyumbishwa na mwanaume. Akipiga stori na Risasi Vibes, Shamsa alisema kuwa anamshukuru Mungu kwa kumpa akili ya kujitambua na kujua yeye ni nani, hivyo ndio maana siku zote anapambana mwenyewe ili apate pesa zake na sio kutegemea mabwana.
“Naijua thamani yangu, zaidi najitambua sana, namshukuru Mungu kwa hilo, ndio maana napambana kila siku kutafuta pesa yangu ili baadaye nisije kuwa tegemezi kwa mwanaume. Hivyo nawashauri na wanawake wengine kujitambua ili wasiyumbishwe na waume zao,” alisema Shamsa ambaye amemwagana na mumewe, Chid Mapenzi.