Sitaki Mwanaume Asiyekuwa na Pesa' - Lulu Diva


Msanii wa Bongo Fleva Lulu Diva amesema hajawahi kuhongwa, wala kujihusisha na kimapenzi na mtu ajipatike kipato, ila amesema hawezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kumuhudumia.


Lulu Diva ametoa kauli hiyo akiwa anazungumza kwenye kipindi cha Kikaangoni cha EATV cha kila Jumatano kuanzia saa 8 : 30 Mchana, ambapo amesema tuhuma za kudanga si kweli.

"Kiukweli sijawahi kudanga, ila kuhusu gari ninayoitumia nilipewa na mpenzi wangu wakati wa birthday yangu, kwa hiyo nikipewa na mpenzi wangu siwezi kusema ni kudanga." amesema Lulu Diva

"Mimi sijawahi kudanga, ila siwezi kuwa na mwanaume ambaye hawezi kunihudumia, siwezi kuwa na Mario, mwanaume ambaye hana kazi hata nikimwambia nina tatizo hili, hawezi kunisaidia" amesema Lulu Diva

Kwa sasa Lulu Diva anatamba na ngoma ya Chekecha
Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mmezoea maisha ya kubebwa ndiyo maanabunaongea hivyo, wewe ni aina ya wanawakw wasiopenda kujishughulisha na kazi za kujiingizia kipato, elewa mapenzi siyo hela ndiyo maana Mungu aliumba mtu mume na mtu mke ili washirikiane.

    ReplyDelete
  2. Kauli yako tu inaonyesha ni mwanamke unayependa hela kupita kiasi na unapenda raha na kuishi maisha ya anasa, wewe ndiye aina ya wanawake ukiweka ndani hawezi hata kuandaa chai ya mume wake asubuhi.WanaumeWenzanguMsioeWanawakeWaAinaHiiOvyoKabisa.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad