Soma Hadi Mwisho...Mungu Wetu Anaweza Tukiomba na Kusali...
2
April 18, 2020
MAMA mmoja aligunduliwa kuwa na Virus Vya Corona, alichukuliwa hadi kwenye hospital ya wagonjwa wa ugonjwa huo unaendelea kuitesa dunia.
mama huyo baada ya kufikishwa hospital
madaktar walimfanyia vipimo kwa mara nyingine, jambo la kusitikisha ni kwamba, madaktari wale waligundua mama yule hana uwezekano wa kupona, kwani corona ilishamuathiri kwa kiwango kikubwa sana. ana saa4 za kuvuta pumzi,
namaanisha amebakiza masaa 4 apoteze maisha,kwani licha ya kuwa na corona, pia alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kisukari ulimpoteze kinga nyingi za mwili.
mama huyo alianza kulia kwa uchungu, ni baada kuambiwa hana nafasi tena ya kuendelea kutembea juu ya dunia, madaktar walimuacha hawakumpa dawa wala kumuhudumia kwa chochote, walimtelekeza mama huyo na kwenda kuhudumia wagonjwa wengine wenye uwezekano wa kupona huku wakisubiri mama huyo afe waje kutoa mwili wake kitanda alichokalia kiwekwe mgonjwa mwingine, kwani wagonjwa waliokuwa wanaletwa hospital hapo ni wengi mno.
"Sina matumaini ya kuishi Tena, Nakufa Mimi..." alisema yule mama huku akilia. lakini badae mama huyo alijiwa na matumaini ya kuendelea kuwa hai, ni baada ya kukumbuka mbinguni kuna MUNGU asiyeshindwa na lolote lile, Mama Yule Alipiga Magoti Chini Na Kuanza Kumlilia Mungu, akimuomba amponye ugonjwa anaumwa.
"Eee Mola Wangu Ukinichukua Mimi Nani Atakuwa Msaada Kwa Watoto Wangu? Niokoe Na Mauti, Niongezee Muda Wa Kuishi Bado Nahitajika Kwa Wanangu, Usiache Niangamie, Niokoe Mola Wangu, Hakika Mimi Ni ninakutegemea wewe, na Miongoni Mwa Wenye Kukuabudu..." Ni baadhi ya maneno yaliyomo kwenye maombi ya mama huyo, Aliyatamka huku akilia.
Hatimae Saa 4 Alizokuwa amebaki nazo Yule Mama zilifika na zikapita, madaktar walikuja kuchukua maiti lakini walikuta yule mama hajafa bado ni mzima, wakarudi na machela yao ikiwa tupu, kesho yake walikuja na machela yao, wakiamini tayari yule mama amesha kufa, lakin walimkuta bado Ni mzima, tena akionekà na kuwa mchangamfu zaidi ya Jana, Madaktar wale waliangaliana kwa mshangao, hakuna aliyejuwa Siri ya mama yule kuendelea kuwa hai Hadi mda ule, wakati vipimo vyao vilionyesha Mama Hana mda mrefu wa kuishi.
Madaktar walimsogelea mama na kumfanyia vipimo kwa Mara nyingine, hapo ndipo madaktar walizidi kuvishangaa vipimo vyao kwani vilionyesha Mama huyo haumwi Tena Corona wala kisuri.
"Mama umeponaje Hali ya kuwa sisi hatujakupa dawa yoyote?" Aliuliza Daktar mmoja, Mama yule alishinda kujibu swali hilo, Alianza kulia kwa furaha, akawaambia wale madaktar "MUNGU WETU ANAWEZA"
Hatimae Mama huyo aliruhusiwa kurudi nyumbani akiwa mzima wa Afya, watoto walimpokea Mama yao kwa furaha.
Ukiishi kwa kumtegemea Mungu utaishi kwa furaha Sana.
Mungu wetu ni anatupenda, anasikiliza maombi yetu na kuyajibu, Unapomuomba MUNGU na akaona unachelewa kujibiwa maombi yako, usichoke Endelea kuomba ipo siku utajibiwa, Mungu humjibu amtakae na kwa wakati aupendao.
Usisubiri umepatwa na tatizo ndio uanza kumuomba MUNGU akuondolee matatizo, Anza kuomba leo kabla haujapatwa na matatizo, muombe akukinge na matatizo, kwani siku zote kinga Ni Bora kuliko tiba.
Kwa pamoja tunamuomba Mungu muumba mbingu na Ardhi atuondolee Corona, Tanzania na Duniani kwa Ujumla.
Atulinde dhidi ya Magonjwa na Walimwengu wabaya.
NEEMA YA MOLA IWE NAWE DAIMA.
KAMA HAUPO BIZE UNAWEZA KUCOMMENT "AMEN"
Tags
Allah ni muweza wa yote.
ReplyDeleteblog my earlier comment pls.
Ramadhan Kareem
Ni ukweli usiopingika. Kila mmoja kwa
ReplyDeleteiimani yake.
Allah ni muweza wa yote, Mleta Uhai na Muondosha Uhai.
Mfalme wa Wafalme wote.
Muweza asie wezekana.
Hakimu wa Mahakimu.
Muumba wa tunavyo viona na Tusivyo Viona.
Inapasa kumtii na kuuabudu kwa Haki.
Angalia kwa uwezo wake Italy kwa muda mfupii waliopoa si chini 2500 hizi zote ni Kudra na Dalili za Mwenyezi Mungu.
Tuendelee kumuomba. usiku na mchana Atuepushe na Janga hilina mengineo tuna yaua na tusio yajua.
Allah ni mwingi wa Rehema n msamehevu.