Taharuki Mondi Kuporwa Wasafi



Taharuki imetawala! Hivi karibuni zimeibuka tetesi kwamba, staa wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ au ‘Mondi’ amepokonywa hisa za umiliki wa Kampuni ya Wasafi Media Ltd yaani Wasafi FM na Wasafi TV, Gazeti la IJUMAA limeichimba kwa undani habari hiyo na kuibuka na majibu kamili.

 

TAARIFA ZA AWALI

Taarifa za awali zilizotoka kwenye dawati la IJUMAA zilieleza kuwa, Mondi alikuwa hana maelewano mazuri na wanahisa wenzake kwenye kampuni hiyo, hivyo wameamua kumlipa kiasi chake na kumtoa kwenye kampuni.Gazeti la IJUMAA linafahamu mbali na Mondi, kwa upande wa Wasafi TV, kuna wafanyabiashara wengine wawili akiwemo Joseph Kusaga ambaye pia ni mmiliki wa Clouds Media Group.

 

TANGAZO LA TCRA

Kwa mujibu wa tangazo la Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), wamiliki wa Wasafi TV ni Zaghalulu Ajmy anayemiliki asilimia 53, Mondi (asilimia 45) na Ali Khatib Dai (asilimia 2).

 

REDIO GIZA NENEKuhusu redio, hakuna taarifa zilizowahi kuwekwa wazi, hivyo kuwepo kwa ugumu wa taarifa hizo. 

CHANZO CHAMWAGA UBUYU

Chanzo makini kililitonya Gazeti la IJUMAA kuwa, mchakato wa kisheria umeshafanyika na Mondi hana chake tena kwenye kampuni hizo.“Nasikia bwana Diamond si mmiliki tena wa Wasafi FM na Wasafi TV, mambo ya kisheria yameshafanyika, inasemekana kuwa amepewa shea (hisa) zake alizokuwa amewekeza, Mondi alikuwa anajitapa sana kwa watangazaji wake na kwa sasa siyo bosi tena,’’ kilidai chanzo hicho kilichofikiwa na Gazeti la IJUMAA.

 

Habari hiyo ilizua taharuki kubwa kwa watu wote waliofikiwa na uchunguzi wa gazeti hili ambapo wengi walisema, itakuwaje sasa kama Mondi amevuliwa hisa hizo wakati media hiyo inafahamika kwa jina lake la Wasafi?“Sijui sasa itakuwaje kama wataendelea kuiita Wasafi Media! Diamond naye ataridhika au ataanzisha kampuni nyingine ya media?” Alihoji mmoja wa watu aliyefikiwa na uchunguzi.

 

MFANYAKAZI AONGEA

Mbali na chanzo hicho, IJUMAA lilizungumza na mmoja wa wafanyakazi wa ‘midia’ hiyo ambaye hakupenda jina lichorwe gazetini ambaye alikiri kuwepo kwa madai hayo.“Mimi nipo hapa muda mrefu na hizo taarifa nimezisikia, ila kiukweli bado sijajua kama zina ukweli wowote au lah, ila tunashukuru shughuli zingine zinaendelea, hivyo kama kutakuwa kuna lolote, basi uongozi utatupa taarifa,” alisema mfanyakazi huyo.

 

UONGOZI WAFUNGUKA

Gazeti la IJUMAA lilifanya jitihada za kumtafuta meneja wa mwanamuziki huyo, Hamisi Taletale ‘Babu Tale’ ambapo baada ya kupatikana alikiri kuzifahamu habari hizo na kusema hazina ukweli wowote, hivyo wamuache mwanamuziki wake atulie na siyo kumpakazia mane ukweli kabisa, halafu hebu watu wamuache basi huyu kijana (Mondi) maana wanamuandama sana, hakuna kitu kama hicho Wasafi,” alisema Tale.

 

MENEJA MWINGINE…Baada ya kuzungumza na Babu Tale, Gazeti la IJUMAA lilimtafuta meneja mwingine wa Mondi, Said Fela ‘Mkubwa Fela’ ambapo naye alisema anashangaa uwepo wa madai hayo.“Unapozungumzia Wasafi ni lazima Nasibu (Mondi) awepo, Fela awepo, Tale awepo na Sallam, sasa nashangaa watu wanaposema hahusiki nayo tena, yaani mtu mwenye chake leo hii umwambie siyo chake kweli?

 

“Mfano mzuri mimi ukiniambia Gazeti la IJUMAA najua mmiliki ni Shigongo, lakini Shigongo yeye ndiye anaweza akawa anawajua watu wake, sasa leo hii nikija kuambiwa Shigongo kanyang’anywa mimi sitawaelewa, Shigongo ananyang’anywaje?



Na kama Gazeti la IJUMAA litaendelea kuitwa IJUMAA au litaitwa Jumapili?“Lakini jina kama bado lako, muanzilishi hata anayeingia hisa, yule mwenye jina au wanaokuja kusema na wao wanataka kuingia, Kusaga yeye ana media inaitwa Clouds pale pana Clouds? Sisi ndiyo waanzilishi, hivyo kama kuna mwekezaji alikuja, basi alikuja kuwekeza, lakini sasa ukisema kanyang’anywa, kanyang’anywa na nani? Hayo ni manenomaneno tu ambayo hata kwenye kanga yapo, TV na redio bado tunavyo.

 

Diamond bado ni mmiliki na ndiye bosi mpaka sasa,” alisema Fella ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Kilungule jijini Dar.

 

TUJIKUMBUSHE

Mondi, baada ya kufanikiwa kimuziki na kupata madili mbalimbali ya ubalozi, miaka kadhaa iliyopita, alifungua studio yake ya kurekodia nyimbo zake kisha baadaye akaamua kuanzisha vyombo hivyo vya habari ambavyo kwa sasa vinatikisa.

 

Vyombo hivyo vimefanya usajili kwa kuwachukua watangazaji katika redio na televisheni maarufu zilizokuwa zimewatangulia ambao wana ushawishi mkubwa, hivyo kuvifanya vituo hivyo kuwa pendwa kwa wasikilizaji na watazamaji wake.

GPL

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad