Tanzia: Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Afariki Dunia



MKUU wa Wilaya ya Mtwara, Wakili Evod Mmanda, amefariki dunia alfajiri ya leo Jumatatu, Aprili 27, 2020, katika Hospitali ya Ligula, Mtwara kutokana na maradhi ya moyo.

Taarifa zinaeleza kuwa aliwahi kulazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili jijini Dar es Salaam miezi minne iliyopita akisumbuliwa na matatizo ya presha kisha baadaye akaruhusiwa.

Mmanda aliteuliwa kuwa mkuu wa Wilaya ya Mtwara na Rais John  Magufuli, Desemba 19, 2016, akichukua nafasi ya Dkt. Khatib Kazungu ambaye alihamishiwa Wizara ya Fedha.

 

Wakili msomi Mmanda aliyekuwa pia mjumbe wa Bunge la Katiba, katika bunge hilo, aliteuliwa na Mwenyekiti wa muda wa vikao vya Bunge Maalumu la Katiba, Pandu Ameir Kificho, kuwa mmoja wa wajumbe 20 ambao walimshauri ili kuboresha utendaji.


Aidha, mwaka 2015 Mmanda alitangaza nia ya kugombea ubunge jimbo la Rombo kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) lakini kura hazikutosha.


Updates:

Mwenyekiti wa Wakuu wa wilaya nchini Daniel Chongolo kwa niaba ya Wakauu wa Wilaya anatoa pole nyingi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, viongozi wote akiwemo waziri wa Tamisemi na wanafamilia kufuatia kifo cha aliyekuwa DC wa Mtwara, Evod Mmanda.

Katibu wa wakuu wa wilaya nchini, mkuu wa wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah ametoa pole kwa wananchi wa Mtwara na wakuu wote wa wilaya kufuatia kifo cha DC Mtwara Evod Mmanda kilichotokea usiku wa kuamkia leo April 27/2020.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad