Katibu Mkuu Shivyatiata Ataja Mchanganyiko Sahihi wa Kujifukiza Kwa Ajili ya Tiba


Katika wakati huu ambao watanzania wengi wanapambana kujifukiza mengi yamekuwa yakielezwa juu ya mchanganyiko sahihi wa kutumia lakini Katibu Mkuu wa Shirikisho la vyama vya Tiba Asilia Tanzania (SHIVYATIATA) Dk Othman Kilamwegula amefunguka juu ya vitu vinavyotakiwa.

Dk Kilamwegula amesema mchanganyiko huo unaweza kusaidia wenye magonjwa ya Homa ya Mapafu, ametaja baadhi kuwa ni Tangawizi limao ndimu na mchaichai ni muhimu kutumia matunda na mboga za majini

Amesema katika kujifukiza kuna mimea ya kuchemsha ambayo ni majani ya mwembe, majani ya mpera, majani ya mkaratusi, ndimu au mchungwa.

Suala la kujifukiza limeibuka kuwa gumzo miongoni mwa watu tangu Rais John Magufuli alipowataka watanzania kuanza kujaribu njia za asili katika kukabiliana na ugonjwa wa virusi vya corona (Covid-19).

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad