Mkongwe wa Bongo Fleva hapa nchini TID, amesema hayupo na hawezi kuwa kwenye mahusiano na msanii wa kike Lulu Diva kwa sababu yeye ni mtu wa zamani na hana pesa.
Akipiga stori na EATV & EA Radio Digital, TID amesema stori hizo za wao kudaiwa kuwa kwenye mahusiano zimekuja kwa sababu wapo karibu sana na watu wanapenda umbea.
"Lulu Diva naongea naye vizuri ila kuna watu wanapenda umbea ila mimi siwezi kuwa naye kwenye mahusiano hata ukiniangalia, mimi ni mtu wa zamani halafu nimetoa wimbo wa zeze mwaka 2000, halafu sina mitonyo na wala sio mtamu wala nini ila anachoheshimu kutoka kwangu ni kipaji" ameeleza TID