TMA Yatahadharisha Mvua Kupiga Mikoa 7 Kwa Siku 5
0
April 13, 2020
Mamlaka ya hali ya hwa nchini (TMA) imetoa tahadhari kwa wakazi wa mikoa 7 ya pwani na kanda ya kati ya Tanzania kutokana na uwezekano wa kunyesha mvua za wastani na kubwa kwa baadhi ya maeneo
Mikoa hiyo ni Dar es salaam, Tanga, Lindi, Morogoro, Pwani visiwa vya Mafia,Unguja na Pemba
Taarifa ya TMA inasema kuwa mikoa hiyo itarajie mvua kubwa na wastani kwa takribani siku tano kwanzia tarehe 12 mwezi April mpaka tarehe 17 April, wakazi wa mikoa hii wanatakiwa kuchukua tahadhari kutokana na hali hii ya mvua
Tangu siku ya jana mkoani Dar es salaam mvua imekuwa ikinyesha kwa takribani masaa kadhaa hali iliyosababisha baadhi ya barabara kufungwa na usafiri kuchelewa
Tags