Trey Songz amuanika mama mtoto wake kwa mara ya kwanza



Staa wa muziki kutoka Marekani, TreySongz kwa mara ya kwanza amemuweka wazi Mama mzazi wa mtoto wake, Noah.

Ni mwaka mmoja sasa tangu mwimbaji huyo atuoneshe sura ya mwanae, TreySongz kupitia ukurasa wake wa Instagram ame-share picha kadhaa za familia yake na kumtambulisha rasmi Mama wa mtoto wake Noah kwa mara ya kwanza huku akiambatanisha na ujumbe wa furaha na pongezi kwa malezi ya mtoto wao.

“Wewe ni mama bora, unashughulia na yote bila matatizo, siku zote nitakushukuru bila uwoga,” aliandika bila ya kuweka wazi jina la Bibie huyo.

Trey ameweza kuikata kiu ya mashabiki zake ambao wengi walitaka kumfahamu ni nani mama wa mtoto huyo licha ya kutokumtaja jina wala kumtag.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad