Trump Aagiza Jeshi la Marekani Kuzilipua Boti za Iran


RAIS wa Marekani, Donald Trump ameliagiza Jeshi la Maji la nchi hiyo (Navy) kuzishambulia na kuziharibu kabisa boti za kivita za Iran pamoja na silaha zake iwapo zinasumbua meli za Marekani na kuongeza usumbufu huko Tehran.

Trump ametoa maagizo hayo leo Jumatano, Aprili 22, 2020 ikiwa ni wiki moja baada ya meli 11 za silaha za Kikosi cha  Iran cha Ulinzi (Iran’s Islamic Revolutionary Guard Corps Navy – IRGCN) kupata matatizo ndani ya bahari karibu na meli za Marekani.

“Nimeliagiza Jeshi la Majini la Marekani kuzilipua na kuziharibu meli zote za Iran zenye silaha ambazo,” Trump ameandika katika akaunti yake ya Twitter baada ya Iran kurusha satelite yake ya kwanza ya kijeshi angani.

Satellite hiyo imepewa jina la Nour, ambapo maana yake ni mwanga imerushwa kutoka katika kituo cha Qassed katika Jangwa la Markazi na kuizunguka dunia katika umbali wa maili (sawa na kilomita 424.867) huku Iran ikijivunia mafanikio hayo makubwa katika jeshi lake.

“Satellite yetu ya kwanza imerushwa vizuri na imefika salama kwenye obiti yake,’ imesema Iran ikiwa ni baada ya kurusha satelite Zafar mwezi Februari 9, 2020 ambayo ilishindwa kufika katika obiti yake.

Marekani inadai kuwa, meli za Iran zimekuwa zikifanya shughuli zisizo salama karibu kabisa na Meli za Jeshi la Maji za marekani.


Washington imesema satellaitui hiyo imerushwa kinyume na azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu makombora.

Maofisa wa Marekani wamesema kuwa wanahofia huenda Iran inatengeneza mfumo kubeba makombora na mabomu ya nyukilia na kuyapiga popote ndani ya Bara hilo.

Aidha, Iran imekanusha kubeba mabomu ya nyukilia na kwamba urushaji wa satelite hiyo umezingatia azimio la umoja wa mataifa na ni kwa ajili ya shughuli za kawaida za kianga na za amani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad