Trump Awatishia India “Tunataka Chloroquine”



RAIS wa Marekani Donald Trump ametishia kulipiza kisasi dhidi ya India endapo nchi hiyo itapiga marufuku mauzo ya dawa ya Hydoxy-chloroquine, Trump amedai dawa hiyo inaweza kutibu corona, India ambayo ni mzalishaji mkuu wa dawa hiyo Duniani imepiga marufuku dawa hiyo kuuzwa nje.


Rais Trump amesema amezungumza na Waziri Mkuu wa India Narendra Modi na kumwambia kuwa Marekani inataka izipate dawa za Hydroxy-chloroquine ilizoagiza kutoka India ili zisaidie kuwatibu wagonjwa corona na kusema kitendo cha India kupiga marufuku dawa hizo kuuzwa nje hakikubaliki.

Dawa hiyo inatumika kutibu wagonjwa wa Malaria lakini siku za karibuni Trump amekuwa akiinadi kuwa inatibu corona ambapo tayari sasa hivi inafanyiwa majaribio kubainisha iwapo inaweza kutumika kutibu kwa uhakika ugonjwa wa Covid -19 unaosababishwa na maambukizi wa virusi vya corona.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad