Tunda "Nimekua Sasa, Sitaki Mambo ya Mjini"


Tunda: Nimekua Sasa, Sitaki Mambo ya Mjini
MREMBO aliyejipatia jina kupitia kazi ya kuuza nyago kwenye video mbalimbali za wanamuziki wa Bongo Fleva, Anna Kimario ‘Tunda’ amesema ameamua kutulia kwa sababu amekua kiakili, hataki kujishughulisha na mambo ya mjini.

Akichonga na Amani, Tunda alisema kuna wakati mtoto wa kike huwezi kutulia kila wakati macho juu na hata kusumbua wazazi, lakini sasa hivi amejituliza anapanga maisha yake ya baadaye maana amekua na mambo ya kitoto ameyaacha.

“Unajua zamani utoto ulikuwa mwingi sana kwangu mpaka ukapitiliza, kuna wakati nilikuwa sitaki kusikia hata mzazi anasemaje, lakini kwa sasa nimetuliza akili yangu nataka kufanya kitu ambacho kitafanya maisha yangu yasimame,” alisema Tunda.

Stori: Richard Bukos

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad