Umewahi Kutahadharishwa na Mkeo au Mumeo Kuhusu Kuwa Makini na Ndugu yake na Bado Haikusaidia?



Siku kadhaa zilizopita nilikuwa mahali na rafiki yangu mmoja aitwaye Alan (sio jina lake halisi)tunabadilishana mawazo ya hapa na pale. Katika maongezi yetu alianza kunielezea wasiwasi wake juu ya mke wake kutoka na shemeji yake, yaani Kaka yake Alan wa damu toka nitoke.

Alan alinielezea namna ambavyo amekuwa akimuonya mkewe juu ya kuwa makini na Kaka yake yule maana anamjua alivyo kipanga, jambo ambalo anasema Mkewe alionekana kumuelewa na kuahidi ya kwamba atakuwa makini lisitokee hilo analohofia Mumewe.

Sasa jambo linalomtia mashaka Bw Alan ni kila anapofika nyumbani na kupiga stori na Mkewe jina la Kaka yake linatajwa mara kwa mara na Mkewe tofauti kabisa na siku za nyuma.

Mke amekuwa akimuonyesha baadhi ya vitu kwenye simu yake na akimuuliza ameyajuaje basi ataambiwa shem ndio kamuelekeza.

Pia Bw Alan amegundua kwamba sio mara zote Kaka yake huyo anapofika hapo nyumbani mkewe atatoa taarifa, na sababu ni kwamba hata pale Kaka yake anaposema atapitia nyumbani kwa Alan, Mke hasemi mpaka aulizwe tofauti na siku za nyuma.

Sasa kinachomuuma zaidi ndugu yangu Alan ni kwamba hayuko tayari kabisa kusikia kwamba Kaka yake yule "kipanga" anapiga Mke wake, anakiri kabisa ya kwamba moyo wake hauna uwezo wa kuhimili hizo taarifa, anasema akisikia ataanguka chini afe ndio maana hayuko tayari hata kumdadisi Mkewe juu ya hofu yake hiyo zaidi ya kurejea kumuonya mara kwa mara kuwa makini na Kaka yake huyo.

Ushauri unakaribishwa maana hata mimi nimejikuta nipo njia panda.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad