Umri Sahihi wa Kufunga Ndoa ni Huu Hapa
0
April 13, 2020
Kwa mujibu wa utafiti wa Chuo Kikuu cha Utah kilichopo nchini Marekani imebainisha kwamba watu ambao wamefunga ndoa kati ya umri wa miaka 28 mpaka 32 wamekuwa na ndoa yenye mafanikio zaidi.
Utafiti huo umebainisha kwamba ndoa ambazo zipo katika hatari ya kuvunjika ni zile ambazo mmoja wa wanandoa ana umri wa chini ya miaka 20 na wale waliofunga ndoa wakiwa na umri wa miaka zaidi ya 45 na kuongeza kuwa ndoa hizo hazijadumu zaidi ya miaka mitano.
Taarifa za utafiti huo umeongeza kuwa kwa watu ambao wanasubiri kufika umri wa miaka 30 ili kufunga ndoa wanahatari ya kupata shida sana katika miaka mitano ya mwanzo ya ndoa yao
Awali ilijulikana kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri mkubwa ndiyo wananafasi ndogo ya kuachana, lakini utafiti huu umeonesha kwamba watu wanaofunga ndoa katika umri wa miaka 45 uwezekano wa kupeana taraka unaongezeka kwa asilimia 5 kila baada ya mwaka mmoja.
Sababu kubwa inayosababisha watu walio katika umri mkubwa kupeana taraka ni historia za nyuma za kila mmoja wao, imani za kidini, miji wanayotoka, kiwango cha elimu, mahusiano ya kimapenzi waliyopitia awali.
Tags