Unaambiwa Siku Hii Dunia itaponea Chupuchupu Kugongana na Kimondo

Jumatano ya April 29 mwaka huu, dunia itaponea chupuchupu kugongana na kimondo kilichopewa jina Asteroid (52768) OR2 1998 chenye kipenyo cha kilomita 4.1 kilichogunduliwa mara ya kwanza 24 July mwaka 1998 na shirika la utafiti wa masuala ya anga la Marekani (NASA).

Tangu kugunduliwa kwake kimondo OR 1998 kimekuwa kikiikaribia dunia mara kadhaa kutokana na njia yake (orbit) kukaribiana na orbit ya dunia. Mwaka 2004 kilikaribia kwa umbali wa maili milioni 4.5 kutoka uso wa dunia.

Kimondo hicho kinachozunguka kwa spidi ya maili 19,461 sawa na kilomita 31,319 kwa saa au kilometa 8.7 kwa sekunde kimetajwa kuwa hatari zaidi kati ya vimondo vilivyopo angani (most hazardous asteroid on space) na kinaweza kusababisha madhara makubwa kama kitagongana na dunia.

Hata hivyo hakiwezi kugongana dunia kwa sasa. April 29 kitaikaribia dunia lakini kitapita umbali wa maili 3.7 milioni sawa na kilomita milioni 6 kutoka dunia ilipo. Mwaka 2031 kitapita mbali zaidi (kilomita milioni 19) kutoka uso wa dunia na mwaka 2048 kitapita umbali wa kilomita milioni 11 kutoka dunia ilipo.

Kwa mujibu wa NASA, April 16 mwaka 2079 kimondo hicho kitakaribia zaidi kwa kupita umbali wa chini ya kilomita milioni 1 kutoka dunia ilipo. Ukaribu huo utasababisha mvutano unaoweza kufanya kigongane (colide) na dunia, mtikisiko unaoweza kuifanya dunia ihame kwenye orbit yake. Ikitokea hivyo huo ndio utakuwa mwisho wa ustaarabu wa dunia (end human civilization).!

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad