Visa vipya vya Corona Zanzibar, wagonjwa wafikia 12
1
April 13, 2020
Wizara ya afya, Zanzibar leo Aprili 13,2020 imetangaza ongezeko la wagonjwa watatu wa covid 19,na kufanya visiwa hivyo kuwa na jumla ya Wagonjwa 12 kutoka Wagonjwa 9 waliokuwepo awali.
Imeelezwa kuwa wagonjwa hao waliolazwa katika Kituo Maalum cha Matibabu cha Kidimni na kile cha Skuli ya JKU Mtoni wanaendelea vizuri na afya zao zinaendelea kuimarika siku hadi siku
Aidha, Serikali imetangaza kuwa Wagonjwa wawili wamepona na kuruhusiwa kurudi nyumbani huku wakitakiwa kuendelea kubaki ndani bila ya kuchanganyika na watu wengine kwa siku 14.
Tags
Tunaomba serikari yetu mpole macho kwa kiundani zaidi katika swala hili.
ReplyDelete