Rais wa Halmashauri Kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen amesisitiza miito ya uwekezaji mkubwa katika bajeti ya Umoja wa UIaya, wakati jumuiya hiyo ikikabiliwa na athari za virusi vya corona.
Siku chache zilizopita, alipendekeza kufanywa mabadiliko makubwa katika bajeti ya Umoja wa Ulaya ya 2021-2027 ambayo inaweza kuiga mpango mkubwa wa kifedha uliotolewa na Marekani kuifufua Ulaya baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Katika maoni yake yaliyochapishwa kwenye gazeti la Ujerumani la Welt am Sonntag , von der Leyen amesema Ulaya inahitaji mpango mkubwa wa kifedha akisema kuwa mabilioni ya euro ambayo lazima yawekezwe leo ili kuepusha janga kubwa yataviunganisha vizazi vijavyo.
Serikali za mataifa wanachama wa Umoja wa Ulaya zimegawanyika kuhusu hatua za pamoja za kuchukua ili kuepusha athari za kiuchumi za virusi vya corona.