Wabunge 17 Wahofiwa Kuwa na Corona Virus



TAHARUKI imezuka Bungeni baada ya taarifa mbalimbali kuripoti kuwa takriban Wabunge na watumishi wa Bunge 17 wana maambukizi ya Virusi vya Corona nchini Kenya.

Taarifa hizi zinakuja wiki moja baada ya Wabunge, Maseneta na Watumishi zaidi ya 200 kupimwa #Covid_19 ambapo imeelezwa kuwa tayari wameshapokea majibu yao kutoka Wizara ya Afya.

Japokuwa hakuna maelezo ya uhakika kuhusu hili, inahofiwa kuwa Wabunge na Watumishi 17 waliofanyiwa vipimo wamethibitishwa kupata maambukizi ya Corona.

 Hata hivyo Spika wa Seneti Kenneth Lusaka amekanusha madai hayo na kusema sio rahisi kujua ikiwa Wabunge wana maambukizi mpaka pale watakaposema kwasababu kila mmoja alipokea majibu yake mwenyewe.

Amewataka watu kuacha kusambaza uvumi huo na kusema walio na majibu ya vipimo vilivyofanywa ni wahusika pamoja na Wizara ya Afya.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad