Mbunge wa Tarime vijijini (Chadema), John Heche na Mbunge wa Bunda Mjiji (Chadema), Ester Bulaya, wametaka wabunge wote kupimwa ugonjwa wa Corona ili kuondoka hofu.
Heche amesema Naibu Spika ametangaza mmoja wao bungeni amethibitika kuwa na Corona.
“Maombi yangu wizara itupime wote hapa bungeni kujua hali halisi,” amesema Heche katika ukurasa wake wa Twitter.
“Getini tunapita pamoja na ukaguzi na hata canteen. Busara ni wote tupimwe kuondoa hofu,” aliandika Heche
Mbunge Bulaya amesema mara ya kwanza waliomba wabunge wapimwe saivi imekuwa ni shida. “Tulishauri wananchi wapimwe hatukusikilizwa hivi tutamlaumu nani, serikali acheni kiburi watu wanakufa, wagonjwa wanaongezela,’The fact kwamba Naibu spika ametutangazia kwamba mmoja wetu hapa bungeni amethibitika kuwa na Corona... maombi yangu wizara itupime wote hapa bungeni kujua hali halisi..Getini tunapita pamoja, ukaguzi na hata viti canteen. Busara ni wote tupimwe kuondoa hofu.— John Heche (@HecheJohn) April 20, 2020
Tulishauri mara ya kwanza,tunaomba wabunge tupimwe ,sasa ni shida...tulishauri wananchi wapimwe hatukusikilizwa ..hivi tutamlaumu nani ,serikali acheni kiburi watu wanakufa ,wagonjwa wanaongezeka.— ester amos bulaya (@esteramosbulaya) April 20, 2020