Wagonjwa Wa Corona Kenya Wafika 246....Ni Baada ya Wengine 12 Kuongezeka Leo


Kenya imetangaza kuwa na wagonjwa 246 wa corona baada ya kuthibitisha watu 12 wapya wameambukizwa virusi vya ugonjwa wa Covid 19.

Katika taarifa waziri wa afya wa Kenya Mutahi Kagwe, amesema watano kati ya wale walioambukizwa virusi vya corona ni wahudumu wa hoteli na kuongeza kuwa idadi hiyo ilifikiwa baada ya jumla ya sampuli 450 kufanyiwa uchunguzi.

Jana Rais Uhuru Kenyata alitangaza hatua zifuatazo kukabiliana na Corona nchini humo.

1.Wizara ya Afya na huduma za umma itaanzisha hazina ya kuwasaidia wafanyakazi wa Afya wanaokabiliana na mlipuko wa virusi vya corona

2.Wizara ya elimu itachukua hatua kuwalinda wanafunzi kutokana na athari mbaya za hatua zilizochukuliwa kukabiliana na Covid-19

3.Mamlaka ya usambazaji wa tiba nchini Kenya itaondoa masharti ya ununuzi wa vifaa vya kujilinda dhidi ya Covid-19 kwa takriban miezi mitatu ili kurahisishia kaunti kununua vifaa hivyo.

4.Nyumba za watu wasiojiweza jijini Nairobi zitapewa msaada wa fedha na serikali kusaidia familia zisizojiweza

5.Bunge litapitisha tena mapendekezo na miswada kuhusu vichocheo vya uchumi.

6.Polisi atakayekiuka sheria wakati anatekeleza hatua za kukabiliana na usambaaji wa virusi atakabiliwa na mkono wa sheria.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad