Wakenya na Watanzania wavuka mpaka Kinyemela, waperekwa karantini



Iadara ya uhamiaji nchini Tanzania imesema imewakamata Watu 24 wakiwemo raia wa Kenya kwa kosa la kuvuka mpaka kwa njia za panya.

Watu hao na pikipiki 13 walizotumia kusafiria, 10 zenye usajili wa Kenya zimekamatwa mkoani Tanga katika kipindi cha wiki moja (kuanzia Machi 30).

Kati ya waliokamatwa kulikuwa na raia wa Tanzania amabo tuliwarudisha na kupitishwa katika utaratibu wa kawaida ambapo wamepelekwa karantini kwa siku 14 na raia wa Kenya wamerudishwa kwao.

“Watu hao walitumia usafiri wa bodaboda na afya zao hazifahamiki na hakuna anayejiua kwanini wamekwepa uatartibu wa kawaida, ndiyo maana tumewarudisha, Wakenya tumewarudisha kwao ili hatua zichukuliwe huko”.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad