Na Rebeca Duce, Tanga.
Mkuu wa wilaya ya Tanga, Tobias Mwilapwa ,amewataka wananchi wa jiji la Tanga kuacha tabia ya kupuuzia maagizo ya serikali juu ya mapambano didhi ya ugonjwa wa homa ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corana aina ya Covid -19 ili kuepusha maambukizi ya ugonjwa huo.
Mkuu huyo wa Wilaya ameyasema hayo alipokuwa kwenye ziara yake ya muda mfupi ya kukagua maeneo ya standi ya daladala iliyopo Ngamiani na zinazofanya safari zake wilayani Pangani kwamba aweze kujione jinsi ambavyo wananchi wanatekeleza maelekezo yaliyotolewa na serikali ili kupunguza msongamano wa watu na matumizi na vitakasa mikono.
Aidha alisema kwamba kwa hali ilivyo bado baadhi ya wananchi wanafanya mizaha juu ya tahadhari ya ugonjwa wa Corona kwani hawachukulii kwa umakini badala yake wanapuuzia na kufanya utani wakiwa kama watu wasiohusika na maagizo ya serikali.
Sambamba na hayo baadhi ya wananchi wametoa malalamiko yao juu ya uwizi wa koki za ndoo za maji tiriri ambazo zilikuwepo maeneo ya standi ya Nagamiani kwa ajili matumizi ya wananchi wanaotumia usasfiri wa magari hayo na kwamba hakuna namna nyingine ya kutumia maji tiririka.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi hao Bi Rukia ambaye ni Mtendaji kata ya Ngamiani kati amesema wananchi wamekosa majiji titirika baada ya koki zote kuibiwa na watu wasiowapendea mema wananchi wenzao kwani ndoo zote zimekutwa hazina koki na maji hayawezi kukaa tena kwenye hizo ndoo.
Akijibu malalamiko hayo mkuu wa wilaya Tanga Tobias Mwilapwa amewatahadharisha waliofanya uhalifu huo na kusema kwamba ni hujuma inayochelewesha mafanikio ya wananchi juu ya mapambano didhi ya maambukizi ya ugonjwa Corona.
Alisema wapo wafanya biashara ambao wamepandisha bei za koki kutoka sh. 2500 hadi 7000 hivyo waache tabia hiyo na kuhurumia wananchi wa hali ya chini ili waweze kuzinunua kwa ajili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa huo.
Sambamba na hayo alisema kwamba wao kama serikali wakishirikiana wanannchi wenye nia njema tayari wamewabaini watu walioingia nchini kwa njia ya panya wapatao 26 na kwamba kwa sasa wako karantini kwenye shule ya sekondari Usagara kwa ajili ya uchunguzi zaidi mapka itakapofika siku 14 ya uangalizi ili hatua zingine zifutwe za kisheria.