Wanaume Acheni Kulala Kwenye Mageto ya Wapenzi Wenu Ambayo Hamjui Kodi zake Yatawakuta Mazito


Habari ya muda huu msomaji wangu nakukarinisha kakika ukurasa wetu wa mahusiano tuweze kujifunza mambo mbalimbali.

Leo nitaka nikupe mambo muhimu ya kuzingatia nyie wanaume sio kwamba nakutisha ila habari ndio.

Kuna baadhi ya wanaume wako wanapenda kulala kwa wapenzi wao mara kwa mara wakati hata kodi ya nyumba hajui jinsi inavyolipwa yeye hufika na kujilaza akishapewa ule mchezo basi hujiona yupo burudani.

Wanaume jamani mbona mnapenda mdebwedo yatakuja kukuta ya ajabu ukajuta katika maisha yako.

Kwanza mwanaume ambaye anajiamini hawezi kukubali kulala kwenye nyumba aliyopanga mwanamke labda tu kama amehusika kumlipia hiyo kodi.

Najua umenielewa vizuri labda nikupe mfano huu ambao kisa cha kweli kilimtokea huyu kaka ambaye alikwenda kulala kwa huyu mpenzi wake bila kujua kama yupo ambaye analipa kodi yake katika hiyo nyumba.

Mwanaume kufika kajilaza bila hofu yoyote utasema yeye ndio kalipa kodi. Ilivyofika saa tano mlipa kodi kaingia. Naomba unisikilize kwa umakini.

Yule mwanamke ilibidi amuambie ajilaze chini ya kitanda na kumuambia hatachelewa kuondoka kama kumsalimua tu.

Sasa hapo ndio picha lilipoanza mwanaume ambaye ndio mlipa kodi kamuambia analala haondoki. Hapo ujue kuna yule ambaye kajificha uvunguni mwa kitanda anasubiri huyo aondoke.

Yule kaka alilala uvunguni mwa kitanda hadi asubuhi akikusimulia anasema ilibaki robo ajikojolee huku mapigo ya moyo yakimuenda mbio.

Baada ya mlipa kodi kuondoka asubuhi ndipo na yeye akaweza kutoka uvunguni mwa kitanda.

Akisimulia anasema hapo ndio mwisho wa mawasiliano na huyo mpenzi wake na kwamba hatakaa alale kwa nyumba ya mwanamke.

Nimekutolea mfano halisi ili uweze kunielewa ni vizuri ukamchukua mapenzi wako akalala unapoishi kuliko wewe mwanaume kwenda kulala kwa mwanamke.

Kwanza ni hatari kwa maisha yako embu vuta picha yule mwanaume angechungulia uvunguni nini ambacho kingetokea.

Tusipende wanaume kupenda vitu vyake urahisi. Wewe hujawahi hata kuuliza kodi yake hata kusema mwaka nakusaidia kazi yako ni kwenda kula mzigo na kusepa ipo siku yatakukuta na utajutia kupenda rahisi
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad