Watatu Mbaroni Kwa Kumnywesha Mtoto Mdogo Bia na Kisha Kupost Mtandaoni, Yupo Baba



Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga linawashikilia watu watatu kwa kosa la kumnywesha bia mtoto mwenye umri wa miaka mitatu na kisha kumpiga picha na kusambaza picha na video ya tukio hilo kwenye mitandao ya kijamii.

Taarifa hiyo imetolewa leo Aprili 26, 2020, na Kamanda wa Polisi mkoani humo Deborah Magilimba, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ambapo amesema kuwa tukio hilo limetokea siku ya Aprili 24 na miongoni mwa watu watatu waliokamatwa yupo Baba mzazi wa mtoto huyo aitwaye Godius Katisha pamoja na mmiliki wa hiyo Baa.

Biashara ya Ngono..Makahaba Waomba Kuruhusiwa Kufanya Biashara Yao Usiku


"Tunawashikilia wote watatu akiwemo Baba wa huyo mtoto anayeitwa Godius Katisha, na mmiliki wa hiyo Baa kwa kweli wamefanya jambo la kikatili, na tukio hilo limetokea kwenye Baa inayoitwa Bondeni iliyopo Wilaya ya Shinyanga vijijini, walimnywesha pombe mtoto wa kike mwenye umri wa miaka mitatu na kumpiga picha na kusambaza kwenye mitandao ya kijamii" amesema Kamanda Magiligimba.

Aidha Kamanda Magilimba ameongeza kuwa upelelezi utakapokamilika watawafikisha mahakamani.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad