Watu 50 Watoroka Karantini, Watafutwa na Polisi

Kenya
Polisi wanawatafuta watu 50 waliotoroka katika Kituo cha Kenya Medical Training College, mjini Nairobi kilichokuwa kinatumika kama karantini

Inadaiwa kuwa walikuwa wanapata chakula cha jioni, na mvua ilikuwa inanyesha ndipo wakatumia fursa hiyo kuruka uzio na kukimbia

Wengine kati ya hao waliotoroka walikuwa wanasubiri majibu ya vipimo vyao kama wana #CoronaVirus, na walikuwa katika uangalizi iwapo wangeonyesha dalili yoyote ya kuwa na virusi hivyo

Hadi hivi sasa Kenya ina jumla ya visa 296 vya #COVID19. Huku watu 92 wakiwa wamekamatwa na watawekwa karantini kilazima baada ya kukiuka sheria ya kukaa umbali wa mita moja

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad