Watu laki moja wamefariki hadi sasa na virusi vya corona duniani kote


Zaidi ya watu 100,000 wamefariki hadi sasa kutokana na virusi vya corona, kwa mujibu wa tarakimu zilizotolewa na chuo kikuu cha Johns Hopkins. Kumekuwa na kesi 1,650,000 zilizothibitishwa za maambukizi duniani kote.

Wasafiri wanaoingia Ujerumani kutoka nje wanatakiwa kuwekwa katika karantini kwa muda wa wiki mbili chini ya sheria ya kuzuwia maambukizi zaidi ya virusi vya corona nchini humo.

China bara imeripoti maambukizi mapya ya watu 45, ikiwa ni ongezeko kutoka watu 42 siku moja kabla.

Maafisa mjini Moscow nchini Urusi, wataanza kutoa vibali kwa watu ambao bado wanataka kutoka majumbani mwao huku kukiwa na hatua ya kufungiwa, na kuanzia na wale wanaokwenda kazini.

Uturuki imeanza marufuku ya kutembea usiku katika miji 31 nchini humo kuanzia usiku wa manane jana Ijumaa katika juhudi za kudhibiti maambukizi ya virusi vya corona nchini humo.

Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus , ametahadharisha kuwa kuondoa hatua za kuzuwia kusambaa kwa virusi vya corona kabla kunaweza kusababisha kurejea tena kwa virusi hivyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad