Watu wa Nne Washikiliwa kwa Tuhuma za Kumkata Visu Rafiki yao


Na Amiri kilagalila,Njombe

Jeshi la polisi mkoani Njombe linawashikilia vijana wanne kwa tuhuma za kumpiga sehemu mbali mbali za mwili na kumkata visu rafiki yao baada ya kunywa pombe iliyonunuliwa na wenzake bila yeye kulipia chochote.

Kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issa amesema tukio hilo limetokea kijiji cha Igominyi tarafa ya Njombe mjini.

“Kulikuwa na vijana wapatao watano ambao walikuwa wanafanya kazi eneo moja la kupasua mbao wakaamua kwenda kujifurahisha kwenye kirabu cha pombe za kienyeji,kuna mwenzao mmoja akawa anakunywa pombe za wenzake huyu anaitwa Godfrey Mbuligwe”alisema Kamanda Hamis Issa

Ameongeza kuwa
“Godfrey Mbuligwe huyu ni mkazi wa Mafinga kitendo cha kunywa pombe za wenzake na wenzake wakachukia na walichokifnaya walimpiga sehemu mbali mbali za mwili na walimkatakata visu”alisema tena Hamis Issa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad