Waziri aeleza hali ya Mwana Fa, mmoja hayuko sawa



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema kuwa hali ya mwanamuziki wa Hip Hop Mwana Fa, inaendelea vizuri kwa sasa na kwamba yuko anaendelea na mazoezi yake ya kila siku.

Waziri Ummy ameyabainisha hayo leo Aprili 7, 2020, wakati akimkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, vifaa mbalimbali vya kujikinga na maambukizi ya Virusi vya Corona, ambapo licha ya kuwa wagonjwa wote walioko karantini kuendelea vizuri, lakini amekiri kuwepo kwa mgonjwa mmoja ambaye hali yake siyo nzuri.

"Katika kesi hizi 24 zilizopo, wagonjwa 18 wote wanaendelea vizuri, lakini ninataka kukiri na niseme wazi kuna mgonjwa mmoja tu ambaye yuko 'unstable', lakini wengine wote wako vizuri na wanafanya kazi zao kina Mwana Fa wanapiga push up tu" amesema Waziri Ummy.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad