Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Jonhson alazwa hospitali akionyesha dalili za virusi vya corona


Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson amelazwa hospitalini ili kufanyiwa vipimo vya virusi vya corona, siku 10 baada ya kukutwa na virusi vya ugonjwa huo, ofisi yake ya Downing Street imesema.

Alikimbizwa katika hospitali moja ya mjini London siku ya Jumapili akionyesha dalili za virusi hivyo ikiwemo kiwango cha juu cha joto mwilini. Imedaiwa kuwa hatua hiyo ya tahadhari ilichukuliwa kutokana na ushauri wa daktari wake.

Waziri mkuu bado ndie msimamizi wa serikali, lakini waziri wa maswala ya kigeni nchini humo anatarajiwa kuongoza mkutano wa virusi vya corona siku ya Jumatatu.

Hatua hiyo inajiri baada ya malkia Elizabeth kulihutubia taifa akisema kwamba Uingereza itafanikiwa katika vita vyake dhidi ya mlipuko wa virusi hivyo.

Katika hotuba isio ya kawaida , mfalme huyo aliwashukuru raia kwa kufuata maelezo ya serikali kusalia nyumbani huku akiwapongeza wale waliojitolea kuwasaidia wengine.

Pia aliwashukuru wafanyakazi muhimu akisema kuwa kila saa la kazi linazidi kuirejesha Uingereza katika hali yake ya kawaida.

Hotuba hiyo inajiri huku idadi ya watu waliofariki kutokana na virusi hivyo nchini Uingereza ikipanda na kufikia 4,934.

Akizungumza katika jumba la kifalme la Windsor, malkia huyo alisema kwamba tumekumbwa na changamoto nyingi katika siku za nyuma lakini hii ni tofauti.

Aliongezea kwamba wakati huu tutaungana na mataifa mengine duniani kwa kutumia hatua za kisayansi zilizopigwa ili kujiponya. tutafanikiwa na kwamba ufanisi huo utakuwa wa kila mtu.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad