Watu wengine 11 wamegundulika kuwa na virusi vya Corona nchini Kenya na kufanya idadi ya maambukizo kufikia watu 208.
Mtu mmoja pia amethibitishwa kufariki ndani ya saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya vifo vinavyotokana na virusi hivyo kufikia watu tisa.
Kwa mujibu wa waziri Kagwe wagonjwa wapya 11 wote ni raia wa Kenya kati yaowanawake sita na wanume watano.
Wanne kati yao walikuwa wamesafiri kutoka Falme za Kiarabu (UAE) huku waliosalia wakiwa hawana historia ya kusafiri.
Pia takriban wagonjwa 15 waliokuwa wakiugua virusi vya corona nchini humo wamepona katika kipindi cha saa 24 zilizopita na kufanya idadi ya waliopona kufika 40.