WHO yaonya Safari Bado Ndefu Katika Mzozo wa Virusi vya Corona



Shirika la afya duniani WHO, limeonya kuwa mzozo uliosababishwa na janga na virusi vya corona hauna dalili za kuisha hivi karibuni, likisema mataifa mengi ndiyo kwanza yako katika hatua za mwanzo za mapambano, huku idadi rasmi ya vifo duniani ikipindukia 180,000.

Wakati baadhi ya mataifa yakianza taratibu kuondoa vikwazo vilivyosimamisha maisha ya kila siku duniani, mkurugenzi mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus ametoa onyo hili. "Majanga mengi katika Ulaya Magharibi yanaonekana kutulia au kupungua. Ingawa tarakimu ni ndogo, tunashuhudia ongezeko barani Afrika, Amerika ya Kati na Kusini, na Ulaya Mashariki.

Na baadhi yalioathirika mwanzoni mwa janga hli sasa yanaanza kushuhudia kuongezeka tena kwa visa. Tusifanye makosa: Bado tuna safari ndefu. Kirusi hiki kitaednelea kuwepo kwa muda mrefu," alisema Tedros.

Mataifa mbalimbali yanachukuwa hatua za kukabiliana na janga hilo ambalo limewauwa zaidi ya watu 180,000 na kuwaambukiza zaidi ya milioni 2.6 duniani, huku yakihaha kutafuta njia ya kupunguza madhara ya kiuchumi.

Lakini Ujerumani, ambayo imeanza kufungua shughuli za kiuchumi kwa tahadhari, imetoa matumaini kwa kutangaza kuwa majaribio ya chanjo ya kibinadamu yataanza wiki ijayo
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad