Wizara Yatoa Neno Picha za Barakoa Zinazosafishwa

 

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetolea ufafanuzi mzuri kufuatia picha zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii zikionesha watu wakisafisha barakoa zilizochafuka, kitendo ambacho ni kinyume na maelekezo ya namna ya utumiaji wa barakoa hizo.

Ufafanuzi huo umetolewa na Wizara kupitia ukurasa wake wa mtandao wa Twitter na kueleza kuwa picha zinazosambaa si za hapa nchini na kuwataka wananchi kuendelea kujilinda na Virusi vya Corona kama ambavyo imekuwa ikishauriwa.

"Picha hizi si za hapa nchini, tunawaomba Watanzania kuendelea kujilinda na Virusi vya Corona kwa kufuata maelekezo yanayotolewa na wataalam wa afya. Aidha unapohitaji barakoa au vifaa vingine vya afya tafadhali tumia maduka rasmi ya dawa na vifaa tiba yaliyopo kote nchini" imeeleza taarifa hiyo.

Kwa mujibu wa wataalam wa afya imeelezwa kuwa barakoa inatakiwa kutumiwa ndani ya masaa 4-6 na baada ya hapo inatakiwa kuchomwa na moto au kuwekwa sehemu ambayo mtu mwingine hawezi kuichukua na kuitumia tena na wala haitakiwi kufuliwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad