.
Mbunge wa jimbo la Kigoma Mjini Zitto Kabwe amewataka viongozi wakuu wa Wizara ya afya kuiga mfano wa Kenya, Uganda na Botswana katika kulishughulikia suala la mlipuko wa virusi vya corona.
Amewataka Waziri Ummy Mwalimu na Naibu wake Faustine Ndugulile kutoa matamko kamili juu mwenendo wa virusi hivyo kuanzai watu waliopima, waliokutwa na ugonjwa huo, waliopona na waliofariki kila siku.
Aliposti picha ya mfano wa matamko hayo na kuandika hivi “Waziri Ummy na Ndugulile Hapa ni mifano ya matamko ya Wizara za Afya Uganda, Kenya na Botswana kuhusu wagonjwa wa Corona ambapo wanaweka idadi ya watu waliopimwa. Kwanini Tanzania hatuweki idadi ya waliopimwa katika Taarifa zetu? Tafadhali wekeni waliopimwa”
Waziri @umwalimu na @DocFaustine hapa ni mifano ya matamko ya Wizara za Afya Uganda, Kenya na Botswana kuhusu wagonjwa wa #COVID19 ambapo wanaweka idadi ya watu waliopimwa. Kwanini Tanzania hatuweki idadi ya waliopimwa katika Taarifa zetu? Tafadhali wekeni waliopimwa #COVID19TZA pic.twitter.com/T48fIQEBro— Zitto MwamiRuyagwa Kabwe (@zittokabwe) April 8, 2020