Hichi Ndio Alichoongea Diamond Platnumz CLOUDS FM Leo Asubuhi Kipindi cha Power Breakfast

Hichi Ndio Alichoongea Diamond Platnumz CLOUDS FM Leo Asubuhi Kipindi cha Power Breakfast
CEO wa Clouds Media Group @JosephKusaga amezindua kampeni ya BONGE LA MPAMBANAJI ambayo ni maalum kwa ajili ya kuwawezesha Wahudumu wa Afya Tanzania kwa vifaa tiba na mahitaji mengine kwenye vita hii dhidi ya kirusi corona.

Wakati akihojiwa na Power Breakfast ya @CloudsFMTZ Kusaga akasema anao Wapambanaji wenzake ambao wako tayari kuungana na yeye na miongoni mwao ni Vodacom, Tigo na @DiamondPlatnumz ambaye alimpigia simu LIVE na kuzungumza kwenye Power Breakfast.

Akiongea kwenye PB Diamond amesema

“Kwanza nimpongeze CEO Kusaga kwa kuweka nguvu zake kwenye hilo sio kila Mtu mwenye moyo huo, mimi pia nitaweka mchango wangu hapo na kama unavyofahamu tayari pia upande wangu nimeanza kulipia kodi familia zilizokwama kutokana na hii corona”

Baada ya kuzungumzia Bonge la Mpambanaji, CEO Kusaga alimtaka Diamond achague wimbo wake ili uchezwe kwenye PB kuwaamsha Wapambanaji wote ambapo mara ya kwanza alipendekeza apigwe Msanii wake mpya @officialzuchu lakini baada ya Jo kusisitiza kuwa ngoma ya Diamond ndiyo inatakiwa, Platnumz alichagua yope remix na ikapigwa. (via CloudsFM Power Breakfast Cc @officialcza @barbarahassan1 ) #BongelaMPAMBANAJI

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad