Acha Kufanya Maamuzi Kwa Hasira, Utaishia Kujiumiza Mwenyewe Huku Ukichekwa


Nyoka mmoja aliingia kwenye karakana ya seremala. Kulikuwa na msumeno umeanguka chini. Kwa bahati mbaya ulimgusa nyoka, akaumia kidogo. Kwa hasira, nyoka aliung'ata ule msumeno.
Alipoung'ata ule msumeno, aliumia tena (kwa kuwa ni wa chuma). Alipoona anazidi kuumia, akaouna ule msumeno ni adui m'baya sana. Ikabidi atumie nguvu zaidi kuung'ata. Akaamua kujizungusha kwa nguvu kwenye msumeno ule ili aubane na kuunyongelea mbali kabisa.
Masikini... Nyoka yule aliishia kujiua mwenyewe kwa hasira zake juu ya msumeno.

FUNZO:
Katika maisha, mara nyingine tunafanya maamuzi kwa hasira sana kwa lengo la kumuumiza yule aliyetukosea, bila kujua tunajiumiza wenyewe. Tujifunze kusamehe na kudharau baadhi ya watu, matukio, na vitu vilivyotukwaza iwapo kufanya hivyo hakutatuumiza zaidi.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad