Agizo la PAUL Makonda "Hakuna Mbunge Aliyeripoti Inawezekana Hawapo Dar" - Mambosasa


Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, SACP Lazaro Mambosasa amesema kuwa mpaka sasa hivi hakuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwenye ofisi ya Mpelelezi wa kanda hiyo, kutokana na kukiuka kwa agizo la Mkuu wa Mkoa huo Paul Makonda, aliyewapa masaa 24 kurudi Bungeni.

Kamanda Mambosasa ameyabainisha hayo leo Mei 9, 2020, wakati akizungumza na EATV&EA Radio Digital, ilipotaka kufahamu kama kuna Mbunge yeyote aliyeripoti kwa hiyari yake kama ambavyo Jeshi la Polisi lilivyoagiza siku ya Mei 7.

"Hakuna hata mmoja aliyeripoti, inawezekana hawapo Dar es Salaam na ndiyo maana nilisema kama kuna yeyote bado yupo, na hakuna aliyepatikana pia, hatujawasaka lakini ule ulikuwa ni wito" amesema Kamanda Mambosasa.

Hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam alitoa masaa 24 kwa Wabunge ambao wako Jijini humo, waondoke na kurejea Dodoma kuendelea na shughuli zao za Bunge na atakayekaidi basi atakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa nyakati za usiku.

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Mambosasa, Tunashukuru kwa taarifa yako.

    Hawa Watoro kama wameingia Machimbo kuogopa Kauli ya Mh. Makonda basi inawezekana kuwa wako njiani kurudisha Pesa zetu walizo chukua Posho na kusepa.

    Mwangalie nyoka siku zote humshikia mkiani huya unatafuta Kichwa kushughulika nacho.

    Sasa hawa, Ring leader wao ndiyo tumsake kwanza na walibaki ni kama kondoo tu.

    Kuna wawili leo hii wanakuja kuripoti kwa Hiari baada ya kuona Hii Ngoma hawawezi kuicheza na imeshaanza kula kwao.

    Endelea kuchapa kazi Kiongozi wa Kanda Maalumu, Hatuna wasiwasi na utendaji wako toka Ulivyokuwa Jijini Dodoma na Mpaka hapa Darisalama.

    Hongera sana mambosasa kudumisha Amani yetu na Kuwasaka wazururaji.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad