Alichokisema Waziri Ummy Mwalimu Baada ya Ndugulile Kutenguliwa


Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amemshukuru kwa ushirikiano wake aliokuwa akimpa, aliyewahi kuwa Naibu Waziri wake wa Afya, Dkt Faustine Ndugulile, aliyetenguliwa nafasi yake hiyo siku ya jana na Rais Magufuli.

Hayo ameyabainisha leo Mei 17, 2020, kupitia ukurasa wake wa Twitter, na kumkaribisha kwa moyo wa dhati, Naibu Waziri wa Afya mpya Dkt Godwin Mollel, ambaye ameteuliwa siku ya jana.

"Asante Mh Faustine Ndugulile kwa utumishi wako na ushirikiano mkubwa ulionipatia katika kusimamia Sekta ya Afya nchini, kila la heri katika kuwatumikia wana Kigamboni, hongera Dkt Godwin Mollel karibu Wizara ya Afya, naahidi kukupa ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu yao" ameandika Waziri Ummy.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad