Ambrose Dunga: Producer Aliyezivunja Vunja Bongo Records, MJ Records kwa Ma-Beat Makali yenye 'Back Vocals Zake'


Jana usiku wakati nachapa code za JavaScipt (hii language siipendi basi tu!!) huku nasikiliza album ya Joyner Lucas -ADHD kuna wimbo mmoja unaitwa 10 Bands uli-popup. Ndani ya ngoma hii ameshirikishwa the Legend Producer Timberland.



Kwa ambao hamumjui producer Timberland tafuteni ngoma za marehemu Aaliyah (sio huyu wa Wasafi), Aaliyah msanii aliyefariki kwa ajali ya ndege akiwa na crew yake wakitoka ku-shoot video ya "Rock the Boat" kule visiwa vya Bahamas. Karibu 98% ya nyimbo za Aaliyah zilitengenezwa na legendary Timbeland 'Mzee wa Back vocals'.

Karibu nyimbo zote alizotengeneza Timberland, kuna kitu 'common' na very 'unique' kwenye beats za Timberland, zile 'back vocals' ambazo alikua anaimba Timberland mwenyewe. Okey tufanye hivi, tafuta nyimbo zifuatazo sikiliza halafu utagundua nachoongelea:

Aaliyah - Try Again
Aaliyah - Are you that somebody
Aaliyah - More than a woman
Justin Timberlake - My love
Missy Elliott - Get Ur Freak On (Napenda zile back vocals 'Piki piki donsee')
Ginuwine - Same OL G (Aisee ukiwa na stress sikiliza hii ngoma, Timberland nyoko!!)

Sikiliza beats za hizo nyimbo hapo juu. Umesikia hizo back-vocals? Basi huyo ndio Timberland mzee wa ma-beat!

Hii ikanikumbusha miaka ya 2004 mpaka 2012 kipindi Bongo Records na MJ Records bado wanatawala 'music production industry' ya Bongo, kuna producer Mkenya alikuja kuleta mapinduzi akawavunja vunja kina P-Funk Majani na Master Jay wakapotea kwenye production ya muziki wa Bongo-Fleva mpaka kesho!!

Unakumbuka miaka ya 2005 - 2010 karibu kila ngoma mpya ya Bongo-Fleva unasikia wanataja "Mandugu Digitoooo" au wakati mwingine unasikia "41 Recordssssss". Kama umesahau basi sikiliza ngoma ya Prof. Jay "Hapo Vipi" au ngoma ya Mwasiti na Chid Benz "Hao" utasikia hizo jingles. Nyuma ya pazia alikuepo 'Timberland wa Bongo' Ambrose Dunga.

Jamaa kwa muonekano ni kama mshamba mshamba hivi, lakini kazi zake zilikuwa ni nyoko!

Unaikumbuka ngoma ya Nakaaya - Mr. Politician? Basi yule 'Mr. Politician' kwenye video ndio Producer Dunga huyo! Unacheki alivo na msuti ule!! Mshamba kweli.

2401005_1589622816511.png

Fanya hivi, angalia video ya Matonya - Anita pale beat linaanza yule anasema "Tusichongole chongole" ndio Producer Dunga huyo. Umecheki anavookena mshamba na hilo Tishet lake la njano nyuma ya nyumba yenye ukuta wa tofali za kuchoma halafu inataka kubomoka?

2401003_1589622740442.png

Ikafika kipindi wasanii wote waliokua wateja wazuri wa Bongo Records na studio zingine wakawa wanamiminika Mandugu Digital. Producer Lamar nae akaona isiwe tabu, akamkimbia P-Funk ajifie na Bongo Records yake akaenda kuongeza maufundi kwa Producer Dunga. Aisee Lamar na Dunga waliunda 'Duo" moja kali sana.

Akina Prof. Jay wakaona isiwe tabu, wakafuata midundo yenye "back vocals' kwa 'Timberland wa Bongo'. Marehemu Ngwair aliyekua msanii 'Loyal' kwa P-funk na yeye akaona isiwe tabu. Kwanza alikua ameshapotea hasikiki tena, lakin alivoenda kwa 'Timberland wa Bongo' ndipo akaja na "Nipeni Dili Masela" ndio akarudi kwenye mainstream. Hii ngoma ukisikiliza zile 'back vocals' za Dunga utaelewa kwanini Dunga namfananisha na "Timberland wa Aaliyah"

Chini ni baadhi ya ngoma zilizopikwa na producer Dunga akisaidiwa na Lamar (kabla ya kuiva na kuunda 'Fish Crab'):

1. MB Dogg - Natamani (Kule mwishon Dunga anaimba "dumba dumba dumba dumbe")
2. Mwasiti ft. Chid Benz- Hao (Utamsikia Dunga anaimba "Tunadunda dunda duundaaa")
3. Nakaaya - Mr. Politician (Utamsikia Dunga "Nipeni kura zenu.. Nivotieni.. Put your hands up")
4. Prof Jay - Hapo Vipi
5. Ngwair - Nipeni Dili
6. Nako 2 Nako ft Loon - Bayeyo (beat linadunda hili ni nyoko)
7. Matonya - Anita (Tusichongole chongole)
8. Noorah - Baba styles
8. Ngwair ft. TID - She Performs ("Thi..This should be played at high volume")
9. Temba ft. Ray C - Nipe Mimi
10. Fatma ft. Jay Moe - Chozi la kusimuliwa

Kila kitu kina muda wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad