Barakah The Prince Atajwa Kama Msanii Anaowajibu Mashabiki Zake Mbovu Mitandaoni...Naj Aibuka Kumtetea


Mrembo Najdattani amemkingia kifua mpenzi wake ambaye ni msanii Barakah The Prince, kwa kusema sasa hivi amejitafuta na amebadilika kwa kutojibu watu vibaya katika mtandao wa Instagram.


Najdattani amesema hivyo baada ya kuwepo na taarifa juu ya kutajwa kwa mpenzi wake huyo, kwamba ndiye msanii anayeongoza  kuwajibu mbovu mashabiki mitandaoni.

Akizungumza hayo kupitia EATV & EA Radio Digital Najdattani amesema 
"Kiukweli amelifanyia kazi hilo jambo, sidhani kama kipindi cha hapa karibuni amemjibu mtu vibaya kuna muda inatokea kama binadamu, kuna comments zinakukwaza sana hadi ukapoteza muelekeo, huyu sio Barakah yule ambaye mmemzoea kwamba kila kitu kinamkasirisha ndiyo maana amejitafuta kwenye hiyo miaka miwili".

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad