Breaking News: CHADEMA Yazuia Wabunge Wake Kwenda Bungeni.....Yawataka Wajiweke Karantini Kwa Siku 14


Chama cha Demokrasia na Maendeleo- CHADEMA kimetoa maelekezo kwa Wabunge wake wote, kutohudhuria tena vikao vya Bunge vinavyoendelea,na wajiweke Karantini kwa muda wa siku 14 na wasiende majimboni kwao kipindi hiki mpaka pale watakapothibitika hawana maambukizi ya Virusi vya Corona

Taarifa iliyotolewa na  Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe leo Ijumaa May 1, 2020  imetoa maelekezo manne kwa wabunge wa chama hicho ambayo ni; Kutohudhuria vikao vya bunge au kamati za bunge,Kutofika eneo la Bunge Dodoma na Dar es Salaam, Wabunge wajiweke karantini kwa muda wa siku 14, wabunge wa chama hicho wasiende mikoani au majimboni bali wabaki Dodoma hadi itakapothibitika hawana maambukizi

Aidha, CHADEMA  pia wameshauri Bunge lisitishwe kwa siku 21 ili kuruhusu wabunge wote kwenda Karantini, Wabunge wote wapimwe pamoja na familia zao na Kamati za Bunge zifanye vikao kwa njia ya mtandao

Tags

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Kumbukeni Ruzuku na Posho Mtakosa..!!

    Wewe utatokaje Daisalama Mpaka Dodoma Mpaka Moshi na Unaendelea Kukutana na Kujamiika na watu HUKU UKIJUA FIKA MWANAO ANAO.

    WACHENI UENEZAJI KWA LOHO MBAYA.

    BUNGE NDIO LALA SALAMA MLUDI MAJIMBONI MTAFUTE EKA ZA SHAMBA KULIMA AU UFUGAJI ASALI AU UUZAJI MTORI STENDI .

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mdau, Ni Ukweli usiopingika,
      Inabidi yeye awe katika mwendelezo wa kujikakatini mpaka mwezi Julai.

      Hivyo TigoPesa wamesitisha Huduma?

      Kama Huduma Zinaendelea , Basi itapendeza Ruzuku ataipokea Kwa Njia Ya Airtel Money au Mpesa.

      Tafadhali Rudia kujikakatini sio Dodoma eeeeh. Ludi Kijijini.

      Maisha ya Mjini ni Galama.
      Ruzuku na Posho za wenzako Usizikombe... Au kupangisha Chama.

      Delete

Top Post Ad

Below Post Ad