BREKING News:Makonda Atoa Masaa 24 Kwa Wabunge wote waliogoma kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar Warudi Bungeni....,Vinginevyo Watakamatwa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda leo May 06 ametoa Saa 24 kwa Wabunge wote waliogoma kushiriki vikao vya Bunge na kwenda Dar es Salaam  kuhakikisha wanarudi Bungeni tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la Uzururaji.

Makonda amesema kuwa Mbunge anayepaswa kuwa Dar es salaam ni yule mwenye kibali au ruhusa ya Spika wa Bunge, tofauti na hapo ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi Bungeni ili kuepuka kukamatwa.

"Mbunge anayepaswa kuwepo ni yule mwenye kibali cha Spika, kipindi hiki ni hatari na tunataka watu wanaotoka majumbani ni wale wanaoenda kufanya kazi, hatujaalika wazururaji kutoka mikoani, inawezekana wakahatarisha zaidi maisha ya wakazi wa Dar es Salaam kwa kuwaambukiza Corona, kipindi hiki ni muhimu katika Bunge la Bajeti dhidi ya mahitaji ya wananchi" amesema Makonda.

Hata hivyo Makonda amesema kinachomshangaza ni kuona Wabunge hao wamekimbilia Dar es salaam kufurahia maisha, badala ya kwenda majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na mafuriko.
Tags

Post a Comment

1 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. Yessss...!!! Unanikosha Makonda.
    Hawa ndiyo wanataka mchezo wa Uruguay.....

    TENA ASIE NA KIBALI AJISALIMISHE MWEANEYE BILA SHURUTI ...

    DARESALAMA OYEEE.... MAKONDA SAFI..... PAMOJA SANA MH.

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad